July 11, 2018


Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ubelgjiji.

Bao pekee la beki wa kati anayeichezea FC, Barcelona, Samuel Umtiti limeifikisha fainali Ufaransa mnamo dakika ya 51 ya kipindi cha pili kwa kumzidi ujanja beki Marouane Fellaini kuuwahi mpira na kufunga kwa kichwa kupitia kona.

Matokeo hayo yanaifanya Ufaransa sasa kusubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kesho baina ya England dhidi ya Croatia itakayopigwa majira ya saa 3 usiku.

Ikumbukwe Ufaransa ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Uruguay wakati Ubelgiji nayo ikiiondoa Brazil kwa ushindi wa mabao 2-1.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV