July 11, 2018


Na George Mganga

Wakati kikosi cha Yanga kikishuka dimbani leo kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC, mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Sekilojo Chambua, asema hakuna uhakika wa  kufanya vizuri.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia kipindi cha Spoti Leo, Chambua amesema ana mashaka na Yanga kutokana na maandalizi iliyoyafanya kuelekea mechi hiyo kubwa.

Chambua ambaye aliwahi kutamba Yanga enzi hizo, ameeleza Yanga imefanya maandalizi ambayo yana mapungufu ukilinganisha na ukubwa wa mashindano namna yalivyo.

Kutokana na maandalizi kuwa hafifu, Chambua anaamini mechi hiyo itakuwa ngumu akisema Gor Mahia wana timu yenye muunganiko mzuri ukiangalia walikuwa wanashiriki KAGAME hapa nchini iliyomalizika wiki jana.

"Napatwa na mashaka kuelekea mechi dhidi ya Gor Mahia kulingana na maandalizi ambayo Yanga waliyafanya kwakuwa hayaendani na ukubwa wa mashindano, hakuna uhakika wa kufanya vema, mechi itakuwa ngumu" alisema.

Aidha, Chambua amelishauri benchi la ufundi la Yanga kuhakikisha wanawapa wachezaji wao somo la kisaikolojia ili waweze kupata morali kabla ya mechi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic