UTATA WA TOTO KUSAINI KLABU MBILI TOFAUTI, MENEJA WAKE ATOLEA UFAFANUZI
Kukiwa na hali ya utata juu ya usajili wa mchezaji, kiungo Feisal Abdallah maarufu kama Fei Toto kusaini Yanga jioni ya jana huku saa kadhaa zilizokuwa zimepita akitambulishwa na Singida United, Meneja wake Mohammed Kombo, ametolea ufafanuzi juu ya suala hilo.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari, Kombo amesema mpaka kufikia saa 10 ya jana jioni Toto alikuwa mchezaji halali wa JKU na si Singida kama ambavyo vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo na mitandao blog hii vilivyokuwa vimeripoti.
Kombo ameeleza kuwa Singida hawakufanya naye mazungumzo yoyote na ameshangazwa na wao kumtangaza kama mchezaji wao bila kukamilisha taratibu rasmi ambazo zinapaswa kufuatwa ili kupata saini yake.
Meneja huyo amefunguka na kuwatupia lawama Singida kutangaza kuwa wameingia naye mkataba wa miaka mitatu wakati alikuwa ana mazungumzo na Yanga ambao walimuwahi na kufikia nao makubaliano.
Kutokana na sakata hilo, Yanga waliamua kuitisha kikao na Waandishi wa habari baada ya masaa kadhaa kupita wakimtabulisha kiungo huyo akitokea JKU na kuingia naye mkataba wa miaka miwili akiwa pamoja na Meneja wake, Kombo.
Baada ya tukio hilo kuibuka, baadaye Singida United kupitia Mkurugenzi wake, Festo Sanga alikuja kueleza kuwa Toto ni mali yao na tataribu zote rasmi za usajili walizifuata huku akisema utatuzi wa suala hilo wanaiachia TFF na Bodi ya Ligi.
Muwe mbahakiki taarifa zenu,Yanga wamesema amesajiliwa miaka mitatu nyinyi mnaandika ni miaka 2. Acheni ubabaishaji na muwe makini mnachoandika hiyo ni taaluma jamani.
ReplyDeleteMeneja unatupiga kamba, ingekua suala limekaa kimaneno tu tungeamini sasa husemi hizo picha za mchezaji akiwa Singidani ila unaamua kulaumu dobi wakati kaniki ni rangi yake ..............tumeshaelewa ni mchezo wa dau umetumika
ReplyDeleteMeneja huyu asaidie. Mchezaji ambaye yeye ndiye anayemsimamia anaenda kusajili na kupokea pesa Singida United yeye hajui mchezaji anatolewa kwenye media yeye hajui, anasajili Yanga ndipo anastuka na kuwa na mchezaji na kulaumu kuwa Singida hawakufuata viongozi. Je utapeli wa mchezaji unaona sawa? Badala ya kulaani kitendo alichofanya mchezaji ni kibaya, yeye anaona sawa, maadili gani haya?
ReplyDelete