July 13, 2018


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitisha kanuni za kuruhusu usajili wa idadi ya Wachezaji 10 wa kigeni katika Ligi Kuu kuanzia msimu ujao.

Wachezaji hao wanaweza kutumika wote kwa wakati mmoja, katika Ligi Kuu Bara na mashindano ya kimataifa tofauti na ilivyokuwa imezoeleka ambapo timu zilikuwa zinaruhusiwa kutumia wachezaji saba pekee wa kigeni.

Hayo yamewekwa hadharani mchana wa jana na Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia alipoitisha kikao na Waandishi wa Habari kuzungumzia mambo mbalimbali yanayogusia soka kwa ujumla.

Ongezeko hilo la wachezaji wa kigeni linaweza kuwa na faida kwa klabu ya Yanga ambayo ipo kwenye mashindano ya kimataifa pamoja na Simba pia Mtibwa Sugar ambazo zitakuwa zinashiriki michuano ya CAF msimu ujao kuanzia Disemba.

Mbali na maamuzi ya kuongeza wachezaji wa kigeni kutoka saba mpaka 10, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemthibitisha Kidao Wilfred kuwa Katibu Mkuu wa TFF katika kikao hicho kilichofanyika Julai 12,2018 Makao Makuu ya TFF Karume, Ilala.

Kidao amechukua rasmi nafasi hiyo kutoka kwa aliyekuwa na wadhifa huo, Selestine Mwesigwa ambaye ana kesi mahakamani inayohusiana na masuala ya utakatishaji fedha pamoja na aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

1 COMMENTS:

  1. Vizuri kabisa wazawa wajipange kuhakikisha wanapata nafasi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic