July 11, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Azam FC kupitia kwa Ofisa Habari wake, Jaffer Idd Maganga, umesema kuwa umejipanga kikamilifu kuelekea mechi yake ya nusu fainali dhidi ya Gor Mahia FC leo saa 8.

Maganga ameeleza mechi hiyo haitokuwa rahisi kutokana na Gor Mahia wataingia uwanjani wakiwa na lengo la kutaka kulipiza kisasi baada ya kupoteza fainali ya mwisho mwaka 2015.

Ofisa huyo ameeleza Gor Mahia waliweza kuwafunga mabao 2-0 katika fainali ya mwisho ya KAGAME iliyopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam hivyo mechi ya leo itakuwa ni kibarua kizito.

Kufuatia matokeo ya mwisho ambapo Azam alichukua ubingwa, Maganga anaamini watapambana kupata matokeo ili kuendelea kuweka na kulinda heshima ya Azam na katika soka la Tanzania kwa ujumla.

Kuelekea mechi hiyo Maganga amesema wachezaji wote wapo fiti kucheza na hakuna aliye majeruhi, hivyo dakika 9 ndizo zitaamua nani atakayekuwa wa kwanza kutinga hatua ya fainali.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ukanda wa Afrika Mashariki haswa Tanzania na Kenya, itaanza majira ya saa 8 kamili, kisha baadaye saa 11 Simba watakuwa kibaruani kukipiga dhidi ya JKU ya Zanzibar. Mechi zote zitafanyika Uwanja wa Taifa.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic