July 20, 2018



KUFUATIA hukumu iliyomkumba msanii Wema Sepetu ya mwaka mmoja jela au kulipa ya Tsh. Milioni 2, kwa makosa mawili ya kutumia madawa ya kulevya na kukutwa na madawa hayo nyumbani kwake, msanii huyo amelipa faini hiyo mahakamani hivyo hatotumikia kifungo hicho.

Hayo yameelezwa leo nje ya lango la Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar na Wakili wa Wema, Albert Msando ambaye amesema Wema hatotumikia kifungo hicho kwani tayari wameshafanya taratibu za kulipa faini ya milioni mbili kama mahakama ilivyoamuru.
Aidha, Msando amewataka wasanii kutojihusisha na madawa ya kulevya huku akisema kwamba Wema atakuwa balozi mzuri wa kuhimiza vijana na wasanii wenzake kuachana au kutokujiingiza kwenye  matumizi ya dawa za kulevya.
Pia amesema kwamba, kesi ya Wema imekuwa ndefu kwa sababu hakukubari mapema iwapo anatumia madawa ya kulevya kama ilivyokuwa kwa wasnii wenzake wakiwemo TID na Petit Man.

1 COMMENTS:

  1. Ni jambo la furaha Wema yupo huru sasa dada yangu jitulize chapa kazi za maana. Achana na madawa ya kulevya achana nayo kabisa yanawashushia heshima zenu. Wema you are supposed to be a role model lakini si kwa kufanya mambo ya namna hiyo tulia fanya biashara zako halali. Mungu akutunze.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic