July 21, 2018


Nguli wa Chelsea, Gianfranco Zola hatimaye amerejea kwenye kazi ya ukocha ambapo sasa atakuwa msaidizi wa Maurizio Sarri katika kikosi hicho cha Chelsea.

Zola, ambaye aliichezea timu hiyo kwa miaka saba na kufunga mabao 69 kati ya mwaka 1996 hadi 2003, amesha-anza majukumu na wakati akikaribishwa na klabu hiyo yalitumika maneno ‘Karibu Nyumbani Gianfranco Zola’.

Wawili hao wamepewa nafasi hiyo baada ya Antonio Conte kutimuliwa kazi Ijumaa iliyopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic