July 21, 2018


Wachezaji wote wa Yanga unaowajua wewe ambao usajili wao upo CAF jana Ijumaa waligoma kufanya mazoezi huku Kocha Mwinyi Zahera akiwasihi viongozi wawaambie mashabiki wa timu hiyo ukweli.

Zahera alifika mazoezini kwenye Uwanja wa Polisi Kur­asini asubuhi akajikuta yupo na wachezaji watano tena wote ni wageni wengine hata mashabiki wa Yanga hawawa­jui.

Wachezaji wote waliocheza mechi ya Gor Mahia hakuna hata mmoja aliyeonekana mazoezini na Zahera hakuwa na taarifa yoyote lakini Cham­pioni limejiridhisha kwamba wameambizana kugoma kufanya mazoezi wakishinikiza walipwe mishahara yao ya miezi mitatu na kushinikiza pia mashabiki wajitokeze kuokoa jahazi.

Yanga Jumatano ya wiki hii ilipigwa mabao 4-0 na Gorma­hia kwenye mechi ya Shirikisho na timu hizo zitarudiana Dar es Salaam Ijumaa ijayo saa 1.00 usiku.


11 COMMENTS:

  1. duuuuh hii ni aibuu kubwaa ila mjinga

    ReplyDelete
  2. Miezi mitatu hawajalipwa.ndiyo maana walicheza chini ya kiwango Nairobi na kuishia kichapo cha mbwa mwizi!Yanga watapata tabu sana.Poleni

    ReplyDelete
  3. Hivi zamani si kulikuwa na watu wanatekaga timu ikifanya vibaya siku hizi hawapo

    ReplyDelete
  4. Ni ninyi waandishi Wa habari ndio mnaoua timu zetu.Kwa kushindwa kuleta habari making za kiuchunguzi maoema.Shuda ya Yanga haina uongoxi.ni wapiga dili tu

    ReplyDelete
  5. Kwa bipj unsondoa,Yanga tatizo ni uonhkxi haina.waliopo ni wapiga dili tu.( utaiondoa na hii)

    ReplyDelete
  6. Haya Ni mapito tu.hat kwa mtani yakuwakuta Lin yamepita.muhimu mshikamano.ytapita tu..Yanga daima mbele..

    ReplyDelete
  7. Tuwaombee wenzetu kwa sala wakati wao huu mgumu upite kwa heri pasipo kupandisha jazba busara itumike kupunguza hasira na kuleta matumaini ya kuwepo kwa amani ndani ya klabu.

    ReplyDelete
  8. Viongozi wa Yanga waache kukomaaa waeleze ukweli ikiwezekana wawape wawekezaji timu ili mambo yakawe sawa vinginevyo ni aibu tuupu.... Tunakoelekea nikushuka daraja kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic