AKILIMALI ATOA SHARTI KWA MWENYEKITI MPYA YANGA
Katibu wa Baraza la Wazee Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, ametoa sharti kwa Mgombea Mwenyekiti wa klabu hiyo kuelekea uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni.
Licha ya Yanga kuendelea kumtambua kuwa Yusuph Manji ndiye Mwenyekiti wa klabu mpaka sasa, Akilimali ameeleza kuwa anajua mpaka sasa hawana Mwenyekiti huku akishauri ni vema akachaguliwa mwingine.
Akilimali amefunguka na kusema kwa yeyote yule ambaye atawania nafasi hiyo ya juu ndani ya klabu ni lazima afuate katiba ya Yanga ili kuondoa mikanganyiko ya ueledi wa kazi pindi atakapopata nafasi hiyo.
Hatua ya Akilimali kutoa msimamo huo ni kutokana na baadhi ya viongozi kujiondoka kwa sababu zilizotajwa kuwa ni kukosa maelewano baina yao hali iliyosababisha badhi na ya nafasi kukosa wahusika.
Ikumbukwe hivi karibuni, baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ndani ya klabu hiyo waliachia ngazi wakidai kukosa maelewano na uongozi wa juu juu ya uendeshwaji wa klabu hiyo kwonge iliyo na zaidi ya miaka 80.








0 COMMENTS:
Post a Comment