August 28, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia bodi ya ligi (TPLB) imeahirisha mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo zinahusisha klabu za Yanga, Azam na Simba.

Sababu za kuahirishwa kwa mechi hizo ni kutokana na timu hizo kuwa na wachezaji wengi ambao wameitwa kukitumikia kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Mechi hizo ni Azam FC dhidi ya Ruvu Shooting uliopaswa ufanyike Septemba 1 Uwanja wa Azam Complex, Simba na Lipuli uliokuwa uchezwe Septemba 1 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, na mchezo namba 30 kati ya Mwadui FC dhidi ya Yanga uliotakiwa ufanyike Septemba 2 kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Kwa ujumla klabu hizo zimetoa jumla ya wachezaji 15 ambao wataingia kambini Agosti 30 tayari kuanza maandalizi ya kujiandaa na mchezo wa kuelekea kufuzu AFCON utakaopigwa Septemba 8 dhidi ya Uganda huko Kampala.

Baada ya kuahirishwa kwa mechi hizo, Bodi ya Ligi kupitia Mkurugenzi wake, Boniface Wambura, amesema wataangalia tarehe nyingine ambazo watazipangia kwa ajili ya kuzicheza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic