August 28, 2018


Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Bw. Ahamd Ahmadamesema ameridhishwa na maandalizi ya michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON).

Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya  miaka 17 AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Ameyasema hayo Jumatatu, Agosti 27, 2018 wakati akizungumza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Pia ameihakikishia Serikali kwamba hakuna mabadiliyo yoyote ya ratiba yatakayofanyika kuhusu wenyeji wa mashindano na kwamba CAF itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kufanikisha michuano hiyo.

Rais wa CAF yupo nchini kwa ajili ya kuongoza mkutano maalum wa mabadiliko ya katiba ya Baraza la Vyama vya Soka katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam, umehudhuriwa na viongozi wa juu wa nchi wanachama wote 12 wa CECAFA wakiwemo marais.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic