August 26, 2018


Imeripotiwa kuwa Mlinda Mlango wa Manchester United, David de Gea amekataa ofa ya kusaini mkataba mpya ndani ya klabu yake.

De Gea anataka kulipwa mshahara mkubwa zaidi ya Paul Pogba au sawa na Alexis Sanchez ili asaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo.

Kwa sasa De Gea analipwa £200,000 kwa wiki huku Pogba akilipwa £290,000 na Sanchez £400,000.

Kuna uwezekano mkubwa wa Bodi ya Manc United kukaa chini na wakala wa De Gea pamoja na wakal wake ili kuamua hatima ya kumuongezea kiasi hicho cha fedha au la.

Aidha, kwa muda mrefu kipa huyo amekuwa akiwindwa na Real Madrid lakini United wamekuwa wagumu kumuachia kirahisi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic