August 31, 2018




Serikali imetangaza rasmi kupitia Gazeti la Championi Jumatano kwamba Uwanja wa Uhuru unaotumiwa na klabu za Simba na Yanga kwenye mechi za Ligi utafungwa kwa miezi minne.

Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe alitoa tamko hilo kwa mara ya kwanza jana Jumanne kwenye ziara yake katika makao makuu ya Global Group, Sinza Mori Jijini Dar es Salaam.

Mwakyembe ambaye ni msomi wa Sheria, alisisitiza kwamba Uwanja huo wa nyasi bandia utafungwa kupisha ukarabati wa maandalizi ya Afcon kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, inayofanyika mwakani.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano ya Afcon kwa vijana mwakani ambapo nchi mbalimbali za Afrika zitashiriki michuano hiyo huku moja ya masharti waliyopewa ni kuhakikisha  wanarekebisha viwanja kabla ya michuano kuanza.

 “Kuna program maalum ambayo tumeiandaa kwa sasa juu ya kutengeneza viwanja vinavyotarajiwa kutumika katika michuano hiyo, huko nyuma Fifa walitupa fedha nyingi sana lakini hazikutumika vizuri,”Mwakyembe alisisitiza kwenye ofisi za Global ambao ni wachapishaji wa magazeti nguli ya michezo ya Championi na Spoti Xtra linalotoka Jumapili pekee.
“Sasa tuna miaka mitatu hatujapata fedha za Fifa, lakini wameangalia na kugundua kuwa tumeanza kasi ya kupiga vita ubadhirifu na tunaamini kuwa sasa tutapewa.

“Nimeomba fedha kwa ajili ya kuboresha viwanja vitatu vikubwa vitakavyotumika katika michuano hiyo na kufanyia ukarabati ukiwemo Uwanja wa taifa, Uhuru na Chamazi ambapo tutakarabati hadi barabara inayokwenda Chamazi.

“Uwanja wa Uhuru utafungwa kwa muda kama wa miezi minne, kapeti lililokuwepo litaondolewa lote, ukarabati wake utaanza wakati wowote kuanzia sasa,” alisema Mwakyembe ambaye ni mzoefu kwenye masuala ya uongozi.

1 COMMENTS:

  1. Safi sana mh. Waziri pesa ya FIFA lazima itumike kwa malengo husika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic