- • MultiChoice Talent Factory programu maalumu ya kuchochea ubunifu
- • Watanzania 4 kwenda mafunzoni mwaka mzima Oktoba Mosi 2018
Dar es Salaam, Agosti 30 2018. MultiChoice Tanzania, Imetangaza washindi wanne waliokidhi vigezo katika shindano la MultiChoice Talent Factory lilizinduliwa rasmi mapema mwezi Mei mwaka huu . Programu hii itawezesha jumla ya vijana 60 kutoka katika nchi mbalimbali barani Afrika kuweza kupata mafunzo ya filamu kwa kipindi cha mwaka mmoja katika vituo vitatu tofauti, kimojawapo kikiwa nchini Kenya (Nairobi) ambapo vijana hawa watakuwapo ifikapo tarehe 01 Oktoba mwaka huu.
Mchakato mzima wa kupatakana kwa washindi hawa ulichukua takribani muda wa miezi miwili ambapo kwa hapa nyumbani Tanzania tulipokea maombi kutoka kwa vijana zaidi ya 160, yaliyofuatiwa na mchujo ulifanyika tarehe 20 Julai Mwaka huu hapa Dar es Salaam Tanzania.
“Maendeleo ya nchi yetu kwa muda mrefu yamekuwa yakitambuliwa kwa uwekezaji katika maliasili nyingi tulizonazo kama vile madini, kilimo, mifugo, wanyamapori, na kadhalika huku sekta ya ubunifu ikiwa haijapewa kipaumbele kikubwa na hivyo sekta ya sanaa na ubunifu kuwa na mchango mdogo katika ukuaji wa uchumi wetu. Ili kuhakikisha kuwa tunasaidiana na serikali katika mkakati wake wa kuifanya sekta ya ubunifu na sanaa kuwa moja ya mihimili ya uchumi wetu, MultiChoice imeanzisha program hii na tumeanza na sekta ya filamu.
Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, ndugu Alpha Mria akielezea kwa undani namna mchakato huu wa kupata vijana wenye vipaji na mapenzi kwenye sekta ya Filamu na mwisho kupatikana washindi hawa wane ambao mnamo Octoba 2018 wataenda kuiwakilisha Tanzania kwenye ya Mafunzo Maalum ya Tasnia ya Filamu MultiChoice Talent Fatory, huko Jijini Nairobi Kenya kwa kipindi cha mwaka mzima.
Vijana wa kitanzania waliofanikiwa kufudhu katika mchakato huu ni Sarah Kimario kutokea Dar es Salaam, Wilson Nkya kutoka Kigoma, Jamal Kishuli kutoka Arusha na Jane Moshi kutoka mkoa wa Kilimanjaro, alisema Ronald Shelukindo, Meneja Uendeshaji MultiChoice Tanzania.
Tumebarikiwa kwa vipaji vingi katika fani mbalimbali na bila shaka tukiwekeza katika vipaji vya vijana wetu bila shaka tutafanikiwa kupanua wigo wa ajira na uchumi wetu na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.
Amesema mafunzo hayo yataanza rasmi mwezi Oktoba mwaka huu itawawezesha vijana hawa wanne kutoka Tanzania kuungana na vijana wengine kutoka nchi mbali mbali za Afrika katika vyuo maalum vya mafunzo ya utengenezaji wa filamu ambavyo vitakuwa nchini Nigeria, Kenya na Zambia.
Kwa upande wao, washindi waliotangazwa kufudhu katika program hii wametoa shukrani zao za dhati hususani kwa kampuni ya MultiChoice sambamba na serikali ya Tanzania kwa ujumla. Akiongea katika hafla nhiyo, Wilson Nkya mmoja kati ya vijana waliopata fursa hiyo alisema kuwa “ Kipekee hii ni fursa tuliyokuwa tukiisubiri kwa muda mrefu na tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa Kampuni ya MultiChoice, serikali na jamii yote kwa ujumla. Tunaahidi kufanya kila liwezekanalo na mtegemee matokeo chanya kutoka kwetu’, alimalizia Wilson.
Kwa ufupi;
- • Mafuzo rasmi kuanza mwezi wa Oktoba 2018, jijini Nairobi, Kenya
- • Maelezo zaidi yanapatikana kwenye tovuti ya www.multichoicetalentfactory.com
- • Washindi waliochachaguliwa ni wanne (4)
- • Gharama zote zitalipiwa na MultiChoice kwa kipindi cha mwaka mmoja
Tembelea ulingo wa MTF Mitandaoni kwa #multichoicetalentfactory kwa taarifa Zaidi:
- • Instagram: @multichoicetalentfactory;
- • Twitter: @MCTalentFactory
- • Facebook: @multichoiceafricatalentfactory
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na;
Johnson Mshana
Mkuu wa Mawasiliano
0 COMMENTS:
Post a Comment