August 7, 2018


Na George Mganga

Unaambiwa klabu ya Simba si mchezo wa kuuza jezi hapa Bongo kwani tayari ndani ya miaka mitatu iliyopita imeweza kuingiza zaidi ya shilingi, milioni 200 kutokana na mauzo.

Taarifa ikufukie kwamba, kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema Simba wamefanikiwa kuweka rekodi hiyo ambayo ni kubwa kwa klabu za hapa Tanzania.

Aidha, Manara ameeleza kama mipango kwa mwaka huu itakuwa imeenda vizuri, kuna uwezekano wa kutoka kiasi hicho cha milioni 200 mpaka 300 endapo hakutakuwa na ulanguzi wa jezi ambazo wametambulisha jana.

Manara amesema endapo wapenzi na mashabiki wa Simba watanunua jezi ambazo ni asili na si bandia, wataisaidia klabu kufikia lengo la kukusanya kiasi hicho cha fedha ndani ya msimu ujao.

Simba imetambulisha jezi zake rasmi jana ambazo zitatumika kwa msimu ujao ambapo nyekundu zitakuwa za nyumbani na nyeupe kwa mechi za ugenini.


6 COMMENTS:

  1. Ni uongo na wizi mkubwa hivi mnaandika kila mnachoambiwa wamesema ni jezi ngapi zimeuzwa mbeya city walipata milioni 30 msimu mmoja kwa kuuza jezi wakati idadi ya washabiki wao hawafiki hata robo ya washabiki wa simba na hata hivyo jezi zenyewe zinauzwa mkononi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pambana na hali yako wewe siyo kila post lazima u coment

      Delete
  2. 😂😂 simba ni tm kbwa ndo maana inafanya maana kila knavyo kucha

    ReplyDelete
  3. 😂😂 simba ni tm kbwa ndo maana inafanya maana kila knavyo kucha

    ReplyDelete
  4. Ila jezi za mwaka huu hazijanoga kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic