August 21, 2018


Na George Mganga

Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Omary Kaaya, amefunguka juu ya utaratibu mpya uliotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya mapato ya Uwanjani kwenda kwa timu mwenyeji.

Hivi karibuno TFF iliamua kuja kitofauti ambapo mapato ya mchezo husika katika ligi yatakuwa yanaenda kwa mwenyeji badala ya kugawana kama ambavyo ilikuwa awali.

Kwa mujibu wa Radio EFM kupitia E Sports, Kaaya amesema utaratibu unakuwa si mzuri kutokana na timu kutumia gharama za usafiri.

Aidha, Kaaya ameeleza klabu zimekuwa zinatumia gharama za malazi pamoja na chakula hivyo ni vema kama kungekuwa na asilimia 60 kwa mwenyeji na 40 kwa mgeni ili walau kifuta jasho kiweze kuwepo.

Mbali na gharama tajwa hapo juu, Kaaya amesema pia timu huwa zinalipa posho za wachezaji kwa kila mechi hivyo kama utaratibu kama wa zamani ungekuwa unaendelea ungeweza kusaidia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic