August 21, 2018


Mkurugenzi wa Mashindani katika Shirikisho la Soka Tanzania, amesema awamu wanakuja na mtindo wa Play Offs ili kuzisaidia klabu kutomaliza ligi vibaya.

Madadi ameyaeleza hayo baada ya idadi ya klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara kuongezeka kutoka 16 mpaka 20 kwa msimu ujao.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa maamuzi hayo ya kuwa na Play Offs zitasaidia kuepusha upangaji wa matokeo kwenye ligi na kuweka uhalali wa timu ambazo zitashuka daraja.

Madadi amefunguka hayo zikiwa zimesalia siku kadhaa pekee kuelekea Ligi Kuu Msimu ujao ambayo inataraji kuanza Agosti 22 wiki hii.

ikumbukwe ligi hiyo itaanza bila mdhamini mkuu baada ya Vodacom ambaye alikuwa akiidhamini kwa muda mrefu kumaliza mkataba wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic