August 21, 2018


Na George Mganga

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amerejea nchini baada ya kukamilisha kufanyiwa operesheni kubwa ya moyo nchini India ambao ulikuwa ukimsumbua.

Mkwasa amewasili nchini jijini Dar es Salaam na kupokelewa na ndugu zake pamoja na baadhi ya wadau wa soka kisha kuelekea nyumbani kwake kupumzika.

Baada ya kuwasili Mkwasa alieleza kuwa alifanikisha kufanyiwa upasuaji na kumfanya akae takribani siku 3 bila kujua kile kinachoendelea.

Aidha, Mkwasa ameeleza kuwa upasuaji huo ulifanyika kwa takribani masaa sita na wataalam wa Hospitali aliyofikia huko India.

Madaktari ambao walimfanyia upasuaji Mkwasa waligundua moyo wake ulikuwa na matatizo kiasi ambacho kiliepelekea usiweze kufanya kazi kwa muda mrefu.

Baada ya operesheni hiyo kukamilika, Mkwasa amepewa masharti ya kutozungumza na simu na baada ya miezi mitatu anapaswa kurejea tena kwa kufanyiwa vipimo vingine.


2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic