August 23, 2018


Wakati Yanga wakishuka dimbani kukipiga na Mtibwa Sugar leo kwenye Uwanja wa Taifa, Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mkongomani, Mwinyi Zahera, ataendelea kukaa jukwaani.

Zahera atakaa jukwaani kutokana na kukosa vibali vya kazi tangu awasili nchini kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mzambia, George Lwandamina.

Mzambia huyo tangu awasili nchini mabosi wake wamekuwa wakihaha kusaka kibali ili awe huru kufanya kazi kwa asilimia 100 lakini bado mambo hajayakaa sawa.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano, Hussein Nyika, alinukuliwa akisema kuwa suala la ofisi nyingi za serikali kuhamia Dodoma limeleta changamoto ya kufanikisha kibali chake.

Kocha Msaidizi, Noel Mwandila atakiongoza kikosi hicho dhidi ya Mtibwa kuanzia saa 12 za jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tayari kwa kuanza harakati za kuwanyang'anya Simba kikombe ambacho walikitwaa msimu wa 2017/18.

9 COMMENTS:

  1. HII NINI SASA? VIBALI KWANINI HAVIPATIKANI DODOMA HIYO IPO JAPANI AU TANZANIA HII AMBAYO MABASI YA ABOOD YANAENDA KILA SIKU NA KURUDI.HUYU KOCHA MZURI SANA ANAIJENGA TIMU YETU MSIAKE KUMKATISHA TAMAA. MMEONA WENYEWE JUZI MOTO ULIOWAWAKIA WARABU. NI KAZI YAKE YA KAMBI YA MOROGORO.

    ReplyDelete
  2. Hii blog tunaiheshimu lakini haipo fair kwetu sawa tatizo ni la viongozi lakini mwandishi hii taarifa imegeuzwageuzwa Mara ngap kabla ya game utasikia oooh kocha vibali uhakika ikiisha vibali bado hahah unashusha hadhi ya blog yako...

    ReplyDelete
  3. Hii sasa too much viongozi wa yanga muwe serious bas kocha wasimba amekuja juzi tu vibali amepata kocha wetu Ana miezi karibia minne vibali Hana SImba walipataje mapema nyinyi mkakosa viongozi wa yanga tuambieni ukweli acheni utahila basi

    ReplyDelete
    Replies
    1. kuweni na subra....viongozi wanajitahidi kwa uwezo wao.usifananishe kupatikana vibali kwa kocha wa simba na kocha wa yanga kuchelewa.....wangekuwa wanatoka nchi moja kauli yako ndo ingekuwa na nguvu lakini kumbuka ni nchi tofauti na kila nchi ina taratibu zake na u-sharp wake.

      Delete
  4. Hii sasa tunaita too much, hawa viongozi vipi Kocha Simba kaja juzi kapata mna Msaidizi wake! Yapeni umuhimu mambo ya msingi,

    ReplyDelete
  5. Iweje makocha wa simba wanapata vibali vya kazi kiahisi kuliko kocha wa Yanga

    ReplyDelete
  6. Nadhani viongozi wetu kuna changamoto mnayokabiliana nayo ziwekeni wazi ili wanachama au wapenzi wa timu yetu wenye ushawishi na wanaofahamu njia sahihi za kufanikisha upatikanaji wa vibali hivyo wasaidie muda unapita mtamkatisha tamaa aondoke.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic