August 26, 2018


Baada ya maneno mengi huku ndugu wa aliyekuwa mumewe, Amri Athuman ‘King Majuto’ wakidaiwa kumnyima huduma muhimu kama chakula, mjane wa mzee huyo aliyekuwa kinara wa vichekesho Bongo, Aisha Yusuf anadaiwa kutokewa na mzee huyo kwani hafurahishwi na vitendo vinavyoendelea.

Kufuatia madai hayo huku mama huyo akiwa ameondoka Tanga na kurejea kwa wazazi wake jijini Dar, gazeti hili lilimtafuta Aisha ambaye katika mahojiano maalum alielezea hali hiyo;

Risasi Jumamosi: Habari mama, unaendeleaje?

Aisha: Sijambo, naendeelea vizuri.

Risasi Jumamosi: Kuna tofauti gani ya kimaisha tangu Mzee Majuto aondoke?

Aisha: Lazima kuwe na utofauti ingawa ninamshukuru Mungu mimi sijambo.

Risasi Jumamosi: Kuna madai kuwa Mzee Majuto amekutokea hivi karibuni baada ya matatizo yako, je, unalizungumziaje hilo?

Aisha: Hiyo ni hali ya kawaida kabisa kwa sababu mimi nilikuwa karibu naye. Kwa yeyote anayefiwa, atakutana na hali hii ingawa ni mapema mno kuliongelea.

Risasi Jumamosi: Kwa nini unasema ni mapema mno? Je, hakuna chochote amekuambia katika kukutokea huko?

Aisha: Sina la kusema zaidi ya hapo kwani hata watoto bado yupo machoni mwao wanamuona, mara nyingi hata kiimani, kinachoondoka ni kiwiliwili tu, lakini roho bado inakuwepo, kwa hiyo kusema Majuto hajanitokea siwezi kwani namuona wakati wote.

CHANZO: RISASI

3 COMMENTS:

  1. Daaah udaku mpaka kwenye michezo!!! Hizi ni dalili mbaya za kuishiwa. Mwacheni Mzee Amri apumzike kwa amani. Tafuteni habari sio kufufua wafu ili mpige pesa za kilaghai

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic