August 26, 2018


Baada ya Serengeti Boys kuondoshwa kuwania kikombe cha michunao ya CECAFA (U17), na Uganda juzi kwa kufungwa mabao 3-1, baadhi ya mashabiki wa wameiomba serikali kuweka nguvu zake ndani ya kikosi hicho.

Shabiki mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe ameitaka serikali kuwapa nguvu zaidi vijana hao kutokana na vipaji murua ambavyo walionesha mpaka kutolewa na Uganda.

Shabiki ameishauri serikali kuwapeleka Serengeti Boys nchini Sweden ili wakaweke kambi ya miaka 10 kwa ajili ya kuwafanya wawe fiti zaidi.

"Nadhani serikali inapaswa kuweka nguvu zaidi kwa vijana hawa kwasababu wameonesha jambo kubwa licha ya kuondolewa na Uganda"

"Naishauri iwapeleke Sweden wakaweke kambi ya miaka 10 ili waweze kuwa vizuri zaidi baadaye waje kuinua soka la Tanzania" alisema. 

2 COMMENTS:

  1. Nakubaliana na shabiki huyo kwani tumeona vipaji vya vijana wetu vinavyoporomoshwa na hizi timu zetu kwa kutowapa nafasi ya kucheza mfano mzuri ni kipa kabwihili wa ya yanga yupi hadi sasa

    ReplyDelete
  2. Wapelekwe Sweden au Sudan? Umejichanganya kwenye kichwa cha habari umetaja Sweden kwenye habari yenyewe unasema Sudan. Bila shaka umemaanisha Sweden. Mimi sioni jambo hilo kama lina tija lakini pia halitekelezeki.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic