MAKAMBO APEWA RUNGU YANGA
Mshambuliaji mpya wa Yanga, Heritier Makambo, raia wa DR Congo, amepewa jukumu zito la kuibeba timu hiyo katika mchezo wao ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria.
Makambo aliyesajiliwa na Yanga hivi karibuni, tayari Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetoa ruhusa kwa mchezaji huyo kuanza kuitumikia timu hiyo baada ya ishu yake ya vibali kukamilika.
Yanga na USM Alger zinatarajiwa kupambana Agosti 19, mwaka huu ukiwa ni mchezo wa tano wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo timu hizo zipo Kundi D pamoja na Rayon Sport ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya.
Kwa mujibu wa Championi, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, alisema baada ya Makambo kupata ruhusa hiyo, sasa ni wakati wake kuonyesha uwezo uliomfanya akasajiliwa na Yanga.
“Tunangoja Makambo atuonyeshe ubora wake baada ya kuruhusiwa kucheza michuano hii ya Caf, lakini naamini atasaidia timu.
“Si yeye peke yake bali wachezaji wengi wa Yanga wamekuwa wakiisaidia timu kama Ajibu (Ibrahim), Gadiel (Michael), Kaseke (Deus),” alisema Zahera.
0 COMMENTS:
Post a Comment