August 25, 2018


Unaambiwa gumzo kubwa hivi sasa mitandaoni ni kutokana na shughuli ya Mkongomani wa Yanga, Heritier Makambo ambaye ameanza kazi yake kwa kasi kubwa tangu atue Jangwani akitokea FC Lupopo ya Congo.

Licha ya kutupia kambani akiwa Morogoro kwenye mechi za kirafiki, gumzo la Makambo limezidi kuteka vichwa vya habari na kuwashangaza baadhi ya mashabiki wa Simba baada ya kucheka na nyavu za USM Alger kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Agosti 19.

Ukiachana na kuwamaliza waarabu hao kwa bao la ushindi, Makambo alizidi kung'ara zaidi kwa kufunga tena juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar akiweka bao la pili na la ushindi katika mechi iliyomalizika kwa mabao 2-1.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wamoneshwa kushtushwa na kasi aliyoanza nayo Makambo baada ya Yanga kumsajili kimyakimya bila kuonesha mbwembwe.

Mashabiki hao wameanza kuhofia ujio wake baada ya kasi yake ambayo inaonesha itaweza kuwa msaada mkubwa kwa Yanga ambayo hivi karibuni imekuwa na madhaifu kwenye safu ya ushambuliaji.

Baada ya kufanya vizuri dhidi ya USM Alger na Mtibwa, nyota huyo amekabidhiwa rasmi mikoba ya aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Mzimbambwe, Donald Ngoma, ambaye kwa sasa yupo Azam FC.

2 COMMENTS:

  1. hizo habari mnatunga ili muweze kuuza magazeti Simba haiwezi kuchanganyikiwa kwa mtu kama yeye

    ReplyDelete
  2. Makambo peke yake? Kagere, Okwi, Boko, Salamba,kichuya,kaheza.
    Mohamed Rashid. Mfungaji bora wa mabao namba moja wa ligi yupo Simba, namba mbili yupo Simba, namba tatu yupo simba, namba nne kinara wa magoli yupo Simba. Kitu gani kinachowafanya Simba wavugike na mchezaji mmoja?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic