August 25, 2018


Na George Mganga

Baada ya kurejea nchini siku kadhaa zilizopita akitokea India, maendeleo ya hali ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, ni mazuri kwa sasa.

Hivi karibuni Mkwasa alisafiri kuelekea nchini huko kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa moyo ambao kwa mujibu wa madaktari uligundulika kuwa na tatizo la kufanya kazi kiufasaha.

Kwa mujibu wa mke wake na Mkwasa kupitia Radio EFM, Betty Mkwasa, amesema hali ya mume wake kwa sasa inazidi kuimarika japo amekatazwa kuzungumza na simu katika kipindi mpaka muda wake maalum aliopewa umalizike.

Mkwasa alipewa masharti ya kutozungumza na simu kwa muda wa miezi mitatu na muda huo ukishamalizika atapaswa kurejea tena India kwa vipimo vingine zaidi.

Betty ameeleza kuwa mke wake kwa sasa anaendelea na mazoezi ya kawaida ili kujiweka fiti kama ambavyo alishauriwa na madaktari ambao walimfanyia vipimo na upasuaji nchini India.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic