August 27, 2018


Kocha Msaidizi wa klabu ya Simba, Masoud Djuma muda wowote kuanzia sasa ataachana na klabu ya Simba baada ya Klabu ya Simba Kufikia makubaliano kuvunja mkataba.

Taarifa za ndani kutoka bodi ya wakurungezi wa klabu hiyo wamefikia uamuzi huo wa kumuondoa kutokana na kutengeneza mgogoro kati ya wachezaji na kocha mkuu wa klabu hiyo kwa kuwaambia wachezaji kucheza chini ya kiwango ili kocha mkuu afukuzwe na yeye awe kocha mkuu wa klabu hiyo.

Pia Masoud anatajwa kuwa hana maelewanao mazuri na kocha mkuu wa klabu hiyo Patrick Aussems na sasa ni mara ya pili kwa kocha huyo kutoelewana na makocha wakuu wa klabu hiyo kwani hata Pierre Lenchatre alishindwa kuongezewa mkataba mpya sababu mojawapo ni kutokuwa na maelewano mazuri na Masoud Djuma.

Inaelezwa kuwa leo au kesho klabu ya Simba inaweza kutoa taarifa kwa vyombo vya habari ya kusitisha mkataba wa kocha Masoud Djuma ambaye amekuwa kipenzi kwa wanachama na mashabiki wa klabu hiyo Kutokana na sababu hizo mbili.


CHANZO: CHAMPIONI

14 COMMENTS:

  1. Viongozi acheni kutenegeneza migogoro huu si wakati wake,mna uhakika gani kama yeye ndo anawaambia wachezi wacheze chini ya kiwango? kweli mchezaji anayejielewa anaweza kumsikiliza kocha asiye na maamuzi ndani ya timu? mi nafikiri kuna shida hata kwa kocha mkuu ,ila ni mapema sana kuwahukumu.

    ReplyDelete
  2. Thats verry bad bora mzungu aondoke kuliko masoud. Simba hawakuwa na haja ya kocha mzungu

    ReplyDelete
  3. HABARI ZA KICHONGANISHI...KUNA WAANDISHI WAMEPANGWA NA YANGA NA WAO NI WASHABIKI WA YANGA KUNA MKUTANO WAO WALIKAA JUZI MWEMBE YANGA WAKAKUBALIANA MPAKA IFIKAPO TAREHE 30/09 WAME WAMEFANIKIWA KUWAGAWA SIMBA NA KUAKIKISHA WANACHEZA MATCH ZOTE ZA SIMBA ZA MKOANI NA KUNA KAMATI IMETENGWA KWA AJILI YA HILO NA SASA NDO WAMEANZA...DJUMA HANA ISSUE YOYOTE TA UWONGOZI WALA NA PATRICK HAYO NI MAJUNGU YA WAANDISHI WENYE NJAA...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Upuuzi. Yanga bingwa mara 27 ihangaike na simba bingwa mara 19

      Delete
  4. Safi sana uongozi wa simba msilee matatizo

    ReplyDelete
  5. Ukilikoroga utalinywa hakika nakuhakikishia kama Simba watamfukuza Djuma safari yetu ya kutetea ubingwa itakuwa finyu sana tatizo tunathamini sana wazungu but usiache mbachao Kwa msala upitao

    ReplyDelete
  6. Acheni mchezo na pesa..
    Penye pesa lazima migogoro itokee mingi tu..!!

    ReplyDelete
  7. Mafahali wawili hawawezi kukaa zizi moja.Bora Djuma anyanyue mikono maana sioni jipya toka kwake

    ReplyDelete
  8. UONGO MTUPU ACHENI KUWAFITINISHA SIMBA ACHENI WATU WACHEZE MPIRA UMBEYA MTUPU

    ReplyDelete
  9. Huyo mwandishi atunga habari anazitoa wapi, au ilimradi apate wasomaje wengi. badikikeni mtapata tabu Sana

    ReplyDelete
  10. Nimeamin kweli mafahari wawili hawawezi ishi zizi moja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic