Uongozi wa timu ya Mtibwa umefunguka kuwa kwa maandalizi ambayo wanayafanya wana uhakika wa kuitwaa Ngao ya Jamii kwa mabingwa wa Ligi Kuu Simba katika mchezo watakaocheza Agost 18, katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Kocha Mkuu, Zuber Katwila, amesema kuwa wachezaji wana morali kubwa katika kupambana hivyo hesabu zao ni kuhakikisha kwamba wanapata matokeo mazuri yatakayowapa ushindi.
"Mipango inaendelea vizuri kwa sasa na wachezaji na kila kitu kinakwenda sawa hivyo tusubiri na tuone chochote kinaweza kutokea na hesabu zetu ni kuhakikisha kwamba tunashinda na kuweza kuchukua Ngao Jamii.
"Mpira ni sayansi hivyo wachezaji wanajua kazi yao na wana morali kubwa kuhakikisha kwamba wanafanya jambo zuri kwa ajili ya mashabiki wa timu yetu hivyo kila kitu kitakuwa sawa," alisema Katwila.
SOURCE: CHAMPIONI.
0 COMMENTS:
Post a Comment