August 26, 2018


Kichapo cha mabao mawili kwa sifuri walichokipata AFC Leopards ya Kenya katika DABI ya Mashemeji jana kwenye Ligi Kuu nchini humo, kimewafanya wavunje viti jukwaani.

Leopards ambao walimabulia kichapo cha mabao 2-0 waliamua kuvunja viti kufuatia Gor Mahia kufunga bao la pili kupitia kwa Benard Ondiek mnamo dakika ya 38 kipindi cha kwanza na kudai kuwa aliotea.

Kitendo cha hasira hizo za mashabiki kiliwafanya mashabiki wa timu hiyo kuja juu na kuamua kuvunja viti huku wakimtupia lawama Mwamuzi wa mchezo baada ya bao la Ondiek kuzama kimiani.

Maamuzi ya mashabiki hao yanakumbusha kitendo ambacho walikifanya mashabiki wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam misimu takribani miwili iliyopita kwa kuvunja viti baada ya Tambwe kufunga bao huku akiugusa mpira na mkono.

Baada ya ushindi huo, Gor Mahia ainayoongozwa na Kocha wa zamani wa Simba, Dylan Kerr imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi nchini humo na ikifikisha wa taji la 17.

4 COMMENTS:

  1. AMA KWELI WEWE MWANDISHI UMEONYESHA RANGI YAKO HALISI - YOUR TRUE COLOURS

    ReplyDelete
  2. Were mwandishi ni mpuuzi..kwa hiyo hata Misri au duniani kote Fuji zikitokea wanafuata nyayo za simba.Usiandike habari kiushabiki.habari zisizo na busara.

    ReplyDelete
  3. Naam Simba ilipoifunga Mtibwa mbili moja, muandishi huyo aliuelezea kuwa ushindi huo kuwa ushindi mduchu lakini yanga nayo ilipoupata ushindi kama huo kwa timu hiyohiyo ya Mtibwa mbili moja, muandishi huyohuyo, aliisifu yanga kuipa kila aina ya sifa na kuipandisha kileleni. Naam, ushabiki sawa na kikohozi huwezi kukizuwia na ukasahau kila kitu.

    ReplyDelete
  4. Na kama unaona Yanga ndio wameishafanikisha baada ya kushinda mara mbili mfululizo utapata taabu sana.Takwimu za mechi zote mbile haiwabebi zinaonyesha walibahatisha tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic