MCHEZAJI MBRAZIL AJIUNGA NA AL-SHABAB
Mchezaji wa Soka wa Brazil, Wergiton do Rosario Calmon (29) ambaye anajulikana kwa jina maarufu la Somália aliyekuwa akiichezea Klabu ya Toulouse ya Ufaransa kwa miaka mitatu, ametimka klabuni hapo na kujiunga na Klabu ya Al-Shabab nchini Saudia.
Kwa Uarabuni, jina Al-Shabab linamanisha Vijana kwa kiarabu sio jina baya, mitandao ya kijamii ilikuwa na haraka kulishirikisha jina hilo na kundi la kijihad Mashariki mwa Afrika.
Vipo vilabu vingi vya Soka vya Al-Shabaab nchini Syria, Iraq, Kuwait na Oman.
Kundi hilo linalohusishwa na lile la al-Qaeda limekuwa likipigana na serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa kwa, muonhgo mmja uliopita na limetekeleza msururu wa mashambulizi katika eneo hilo.
Somalia amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Klabu hiyo ya Al-Shabaab yenye makao yake makuu yaliyopo jiji la Riyadh.
0 COMMENTS:
Post a Comment