MKONGOMANI YANGA AOMBA URAIA WA TANZANIA ILI AONESHE MAKUCHA YAKE STARS
Zikiwa zimepita siku takribani nne tangu kutangzwa kwa kikosi cha Taifa Stars, taarifa zinaeleza straika hatari wa Yanga, Mkongomani, Heritier Makambo, ameomba uraia wa Tanzania.
Makambo ambaye ameanza katika fomu ya hatari akiwa na kikosi cha Yanga, imeleezwa anajiamini na uwezo alionao huku akijinadi kuwa hawezi akakosa nafasi ya kuichezea Stars.
Taarifa imeeleza kuwa kigogogo mmoja kutoka Shirikisho la Soka Tanzania TFF, amesema kuwa Makambo ameomba afanyiwe mpango huo ili aweze kuungana na Stars tayari ukipiga na Uganda, Septemba 8 2018.
Kigogo huyo ameeleza kama watakamilisha mchakato wa uraia kwa Makambo, jukumu la yeye kuitwa Stars litabakia kwa Kocha Amunike.
Kocha Mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike, alitangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mchezo wa kuelekea kufuzu AFCON dhidi ya Uganda utakaopigwa Uwanja wa Taifa.
Uraia unatolewa kwa mtu wa aliyekaa miezi miwili? Acheni kuvimbisha watu vuchwa bila sababu
ReplyDeleteEti kigogo wa TFF hawa waandishi wa siku hizi
ReplyDelete