August 27, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa unatarajia kuanza safari ya kuelekea Kigali, Rwanda kesho Jumanne kwa ajili kukipiga na Rayon Sports.

Yanga itacheza na timu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambao utakuwa ni wa kukamilisha ratiba pekee.

Kuelekea mchezo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano, Hussein Nyika, amesema kwa namna kikosi chao kilivyo hivi sasa ni lazima kioneshe upinzani.

Jeuri hiyo imetokana na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Agosti 23 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Aidha, Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amesema wanaimani watafanya vema baada ya kuwamaliza waarabu USM Alger baada ya kuwalaza mabao 2-1.

Katika Kundi D, Yanga imefanikiwa kujikusanyia alama 3 ambapo Agosti 29 itahitimisha safari ya michuano ya kundi hilo ikiwa tayari imeshashindwa kufuzu.

2 COMMENTS:

  1. Ni tatu kweli? Sio nne kweli...

    ReplyDelete
  2. Mwandishi tunayoyajua unatudanganya je tusioyajua? Yanga ana point 4 (yanga 0 :0 Rayo Sport ,Yanga 2:1 USMA)

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic