August 27, 2018


Kikosi cha Simba kinashuka dimbani Uwanja wa Taifa leo kwa ajili ya kukipiga na Mbeya City kutoka Mbeya.

Tayari Mbeya wapo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa majira ya saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kuelekea mechi hiyo, Mlinda Mlango, Deogratius Munish 'Dida' atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba baada ya ITC yake kuwasili jana.

Dida aliukosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar pamoja na wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons kutokana na ITC yake kuchelewa kuwasili nchini.

Kukosekana kwake kuliwafanya Aishi Manula na Ally Salim kuendelea kuwepo kwenye orodha ya wachezaji kama makipa wa kikosi cha Simba katika michezo tajwa hapo juu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic