August 27, 2018


Baada ya kung'ara katika mashindano ya CECAFA chini ya miaka 17, straika wa Serengeti Boys, Kelvin John, amesema hana mpango wa kuzichezea klabu za soka Tanzania.

John ambaye amewakonga wadau wengi wa soka la Tanzania na nje kutokana na umaridadi wake akiwa na mpira miguuni, amesema mikakati yake ni kuitangaza zaidi nchi kwa sasa.

John ameeleza kuwa amekuwa akipokea simu na maombi mengi kwa baadhi ya timu hapa nchini ili waweze kumsajili lakini amegoma na kutaka kung'ara nyumbani pia nje ya Tanzania.

Siku kadhaa zilizopitia, taarifa zilieleza kuwa John amevutiwa na klabu ya Manchester United ambaye imeshaanza mazungumzo na wasimamizi wake ili kuweza kumsajili.

Kigogo mmoja TFF ambaye hakupenda jina lake litajwe, alisema United walishaanza mazungumzo kwa ajili ya kumtaka John lakini bado hawajafikiana mwafaka kamili.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic