August 26, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha kuwasili kwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya Mlinda Mlango, Deogratius Munish 'Dida'.

Kwa muujibu wa Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema hati hiyo imeshawasili na kesho mchezaji huyo atakuwa kwenye orodha ya wachezaji wa kikosi cha timu hiyo kitakachocheza na Mbeya City.

Dida hakuwepo kwenye orodha ya wachezaji waliocheza mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar jijini Mwanza Agosti 18 2018 kutokana na kutokuwa na kibali hicho.

Aidha, kipa huyo aliukosa pia mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons uliopigwa Agosti 22 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ukichana na Dida, Manara amesema kuwa ITC ya Mzambia Clatous Chama, ipo njiani na inatarajiwa kuwasili muda wowote kuanzia leo.

3 COMMENTS:

  1. tuliambiwa ITC ya mzambia ipo mara hakuna huyo kiongozi tumueleweje

    ReplyDelete
    Replies
    1. Teaming Sipo Ukweli njiani lakini isije kwa njia ya reli ya Tazara. Hivi tunashindwa kuipata kwa haraka zaidi DHL ili kuwahi mechi kesho jioni tumuone Chama uwanjani?

      Delete
    2. Tuamini tu kwamba ipo kweli njiani lakini isije kwa njia ya reli ya Tazara. Hivi tunashindwa kuipata kwa haraka zaidi DHL ili kuwahi mechi kesho jioni tumuone Chama uwanjani?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic