Baada ya mvutano mkubwa na waajiri wake, kiungo mchezeshaji Mnyarwanda, Haruna Niyonzima atarejea uwanjani na kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake wakati wowote baada ya kuminya pilau la sikukuu ya leo.
Awali, kulikuwepo na sintofahamu ya kiungo huyo anayemudu kucheza namba 8 baada ya kuchelewa kujiunga na kambi ya pamoja ya timu hiyo iliyoweka nchini Uturuki wakijiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
Mnyarwanda huyo alijiunga na Simba kwenye msimu uliopita wa ligi akitokea Yanga baada ya mkataba wake kumalizika wa kuichezea timu ambaye anatarajia kukutana na ushindani kutoka kwa viungo wapya Mzambia, Claytous Chama na Hassan Dilunga.
Championi Jumatano limepata taarifa za uhakika kutoka ndani ya Kamati ya Utendaji ya timu hiyo kuwa viongozi na kiungo huyo tayari wamefikia muafaka mzuri na kumrejesha kikosini kwa ajili ya kuanza mazoezi.
Katika kikao hicho inaelezwa kuwa wamekubaliana baadhi ya vitu baada ya viongozi kukiri kulikuwa na upungufu ikiwemo kwa Niyonzima kuchelewa kujiunga na timu hiyo kabla ya kukubaliana kiungo huyo kurejea mazoezini.
“Niyonzima wakati wowote kuanzia kesho (leo) atarejea uwanjani kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake katika kuelekea msimu mpya wa ligi.
“Kurejea kwa Niyonzima kutaimarisha kikosi chetu kinachoundwa na wachezaji wengi wenye uwezo na uzoefu mkubwa utakaoleta changamoto ya ushindani wa namba,”alisema mtoa taarifa huyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa Gazeti ndugu la Championi Jumatano ambalo ni Spoti Xtra, iliyochapishwa kwenye toleo la Jumapili iliyopita Niyonzima alikuwa na shida nne na viongozi wake.
Gazeti hilo lilitaja sababu hizo kwamba ni kukiuka makubaliano kwenye suala la pango, shule ya watoto wake,uhusiano wake na viongozi pamoja na shinikizo la familia yake.
CHANZO: CHAMPIONI
Wa nini!!!! Ujinga aliokuwa anawaletea Yanga asiulete huku kwetu,kulikuwa na wachezaji mahiri katika timu yetu kuliko yeye lakini hawakuwahi kutuletea ujinga wa namna hii.
ReplyDeleteMNGEMWACHA AENDE ZAKE. MAMBO YA MIGOMO YA WACHEZAJI SIMBA HATUKUZOEA ASIJE TUHARIBIA TIMU YETU
ReplyDeleteTOKA AMEKUJA SIMBA SIJAONA UMUHIMU WAKE UWANJANI. MNEMWACHA TU AOONDOKE KWETU SIMBA HATUNA TABIA YA WACHEZAJI KUSUSA NA KUGOMA SASA KAMA YEYE HIZO NDIZO ZAKE ASIJE AKATUHARIBIA TIMU.
ReplyDelete