August 28, 2018


Kutokana na dua na maombi mengi nyingi kutoka kwa wasanii, mashabiki, jamaa na marafiki wa Msanii Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ambaye yuko nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya matibabu, hatimaye ametoa taarifa juu ya hali yake ya kiafya.

Ikiwa ni saa takribani 24 tangu alipozushiwa kuwa yupo katyika chumba cha wagonjwa mahtuti (ICU) nchini humo, kupitia Insta story yake, Dimpoz ambaye anaendelea na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji wa koo miezi miwili iliyopita, ameandika;

"Ahsanteni sana kwa meseji zenu, alhamdullilah naendelea vyema sana, Inshaallaah kwa uwezo wake Allah nitavuka kipindi hiki kigumu" aliandika.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV