August 30, 2018


Rais John Magufuli ashangazwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingiza makontena 20 nchini yenye samani mbalimbali na kukataa kutalipia kodi akidai kwamba ni msaada kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu kwa mkoa huo.

Magufuli amesema hayo leo wakati akizungumza na watumishi wa serikali wilayani Chato mkoani Geita ambako yuko mapumzikoni.

“Eti Mkuu wa Mkoa ameleta Makontena, ameambiwa alipe kodi, kwa nini asilipe?… Kwa mujibu wa Sheria ya Fedha, Sheria ya Madeni, Sheria ya Dhamana na Misaada ni mtu mmoja tu aliyepewa dhamana ya kupewa misaada kwa ajili ya nchi.

“Umezungumza na watu wengine au wafanyabiashara huko, ukasema una makontena yako halafu unasema ni ya walimu, wala hata shule zenyewe hazitajwi, maana yake ni nini? Unataka utumie walimu ulete hayo makontena, utapeleka shule mbili tatu halafu mengine unapeleka kuyauza.

“Lakini walimu walikwambia wanahitaji masofa, kochi? Wafanyakazi wasitumike kwa maslahi ya watu fulani?” amesema Rais Magufuli.

Makontena hayo yanatakiwa kulipiwa kodi ya bandari kiasi cha Tsh. Bilioni 1.2 ambapo Jumamosi ya keshokutwa yanatarajiwa kupigwa mnada wa pili na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya mnada wa kwanza wa Agosti 25, wateja kushindwa kufika bei iliyopangwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic