August 30, 2018

Kocha mkuu wa Timu ya Tanzania, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amewaondoa wachezaji 6 wa Simba kwa kosa la kuchelewa kuripoti kambini isipokuwa Mlindalango Aishi Manula. Wachezaji hao isipokuwa Manula aliyewahi kambini, walitakiwa kuripoti siku ya Jumatatu baada ya kumalizika kwa mchezo wa dhidi ya Mbeya City lakini walishindwa kufanya hivyo. 

Wachezaji hao ni Nadhodha John Bocco, Shiza kichuya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe pamoja na Hassan Dilunga. Kwa upande wa viongozi wa Simba ambao ni Meneja wa Klabu, Richard Robert , pamoja na Kaimu Katibu Mkuu, Hamis Kisiwa, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa kufuata kanuni limewapeleka kwenye Kamati ya Maadili kwa kutotimiza wajibu wao. Baada ya kuondolewa, wachezaji walioitwa kuchukua nafasi zao ni Paul Ngalema wa Lipuli FC, Salumu Kimenya wa Tanzania Prisons, David Mwantika na Frank Domayo wa Azam FC, Salumu Kihimbwa na Kelvin Sabato wa Mtibwa Sugar na Ali Abdulkadir.

3 COMMENTS:

  1. Tumeona wachezaji wakorofi wengi sana kutoka timu kuu zikiwemo Simba, Yanga, Azam Singida na nyingi nyenginezo, jee tumeona wachezaji hao kufukuzwa kwa kiwango alichotumia kocha huyu mpya na mojakwamoja kuungwa mkono na viongozi wa TFF? Huu jamani ni udhaifu

    ReplyDelete
  2. Nidhamu haijengwi kwa lelemama. Kama wachezaji tunawapenda sana tuwanunulie chai. Timu ya Taifa na Wachezaji kipi bora? Mtu yeyote asiyejua thamani ya muda hawezi kupata maendeleo. Ndio huo unaitwa uswahili. Nampongeza Amunike kwa msimamo huu maana tutofautishe soka na taarabu.

    ReplyDelete
  3. Mimi sio mshabiki wa simba lakini kwa hili si muungi kocha mkono kwa hili.Hajawahi kaa na hawa wachezaji useme wamemusudia pili wachezaji kama kina boko tunawafaham kwa nidham ni miongoni mwa wachezaji wenye nidham ya hali ya juu.Kocha kakurupuka na hili linaenda kumgharimu.Asiangalie tu mpira ndani ya uwanja ajaribu kuwaza kwa mapana zaidi.Alitakiwa kwanza akutane na wachezaji awaambie falsafa zake akiona sasa wachezaji hawazitii ndo achukue hatua.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic