August 30, 2018


Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amepingana na maamuzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuwapiga chini wachezaji 6 Simba katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Rage amesema maamuzi hayo ni ya kuwakosea wachezaji na badala yake akishauri ni vema wangepewa onyo.

Kiongozi huyo wa zamani Simba ameeleza kitendo cha Kocha Mkuu, Emmanuel Amunike kuwapa adhabu kali wakati wakiwa hawana rekodi ya kufanya hivyo si cha busara na badala yake alitakiwa aende nao taratibu.

Aidha, ameshauri ni vema zaidi kama wangeweza kutwafutwa kupewa onyo na ikiwezekana walau kupigwa hata faini jambo ambalo lingewaamsha na kuwa wanawahi kwa siku za usoni.

"Ni jambo ambalo si sahihi kabisa, nadhani wangeweza kufuatwa na kupewa hata onyo kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kuchelewa. Au kama ingewezekana wangepigwa hata faini" alisema.

7 COMMENTS:

  1. Sio kila kitu ni sasa kuna wakati unafika lazima yafanyike maamuzi magumu ili mambo yaende kimsigi alichokifanya kocha Mkuu wa Taifa stars ni sahihi.hii ni nchi huru yenye wachezaji wengi kwenye uwezo na vipaji hivyo kama unakuwa na wachezaji viburi kwanini usichukue wale kwenye kutii mamlaka.

    ReplyDelete
  2. Kanuni zinasema wachezaji wanatakiwa kuripoti siku 3 kabla ya mechi .Kulazimisha ni kutafuta sifa na mgogoro.Kocha akazie uamuzi wake awaache kabisa hao wachezaji ili lijulikane moja.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mechi ni tarehe ngapi?
      Wamechelewa kwa siku ngapi?
      Na wamejulishwa tarehe ngapi kuwa watajiunga na timu ya taifa?
      Na kwa nini wawe ni wa Simba peke yake..?
      Kumbukeni kuwa wachezaji wengi hata mapro huko nje hawapendi kwenda timu ya taifa make kunawavurugia mafanikio yao binafsi..
      Amunike angekuja kwa kujenga hamasa ya wachezaji kutaka kuitumikia taifa stars angeeleweka.. Lakini kwa jinsi anavyoenda tayari Uganda wameshatushinda!!

      Nipo hapa... Mtaniambia!!

      Delete
    2. Iyo ipo wazi Uganda watatufunga tu

      Delete
  3. Naomba msaada kwa wapenda soka wenzangu, nataka kuelewa ni kwa nini wachezaji hawa hawakuripoti kambini? Katibu Mkuu TFF kasema aliwapigia wote simu, kampigia Rais wa Simba, kampigia Meneja wa Timu hadi wakaruhusiwa wajiunge kambini saa 4 za usiku; ni kwa nini hawakwenda isipokuwa Aishi Manula pekee? Ni kwa nini Emmanuel Okwi na Juuko Murshid walishakwenda Uganda? Kwa nini wa Azam waliocheza mechi baada ya Simba walifika kwa wakati?
    Tufanye tafakuri bila jazba tutabaini lipo tatizo!
    Kocha Amunike kaupiga mwingi sana kuliko hao wote.
    Nataka mtu anieleze ni kwa nini Simba imemuweka pembeni kidogo Haruna Niyonzima; siyo kwa mazingara kama haya ya kuchelewa kambini?
    Mchelea mwana kulia...

    ReplyDelete
  4. Kama mpira huu Tanzania hatutafika mbali Co makosa waliofanya wachezaji wa simba walipaswa wapewe onyoa au faini ila kwamaamuzi haya cjuiiiiioo

    ReplyDelete
  5. Manula endelea kuugua na utemwe urudi kundini kwa mechi zetu , tuwaache na taifa stars lao la kocha kuwa na maamuzi kuliko viongozi wa tff

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic