August 30, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba umesema utafunguka kwa kutoa tamko lake Jumatatu ya wiki kesho juu ya wachezaji wake 6 kuondolewa katika kikosi cha timu ya taifa.

Mabosi wa klabu hiyo wameeleza kuwa kwa sasa hawatakuwa na lolote la kusema ili kuepusha shari na badala yake wanasubiria siku ifike watoe neno lao.

Jana kupitia Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wilfred Kidao, aliwataja wachezaji 6 wa Simba kuwaondoa isipokuwa Aishi Manula pekee kutokana na kuchelewa kambini.

Kidao alieleza wamemua kufanya hivyo baada ya Kocha Mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike kukerwa na kuchelewa kwa wachezaji hao kambini.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic