SALAMBA AWEKA REKODI YA AINA YAKE TAIFA
Kama utani vile lakini maajabu yametokea Uwanja wa Taifa jana kwa aliyekuwa straika hatari wa Lipuli FC na sasa Simba, Adam Salamba kucheza takribani dakika 6 bila kufanya maajabu.
Salamba ambaye bado anaaminiwa kufanya makubwa ndani ya wekundu hao wa Msimbazi endapo akipunguza ubishoo, aliingia Uwanjani kipindi cha pili akichukua nafasi ya Nahodha, John Bocco wakati timu yake ikicheza na Tanzania Prisons.
Mchezaji huyo alishindwa kuonesha makeke yake Uwanjani na hii ilikuwa na kutokana na ukomavu wa beki ya Prisons ambayo iliwapa tabu Simba ya kuweza kutikisa nyavu zao.
Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa mapema kabisa na Meddie Kagere mnamo dakika ya pili tu ya mchezo aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia FC.
Baada ya Simba kuanza vema kwa ushindi kiduchu jana, watani zao wa jadi Yanga, leo wanashuka dimbani kuwakaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja huohuo wa Taifa.
NILIJUA MATOKEO YA GOLI MOJA SIMBA HAITAANDIKWA VIZURI JEE KULIKO INGETOKA SARE? AU INGEFUNGWA? NDIO MAANA WACHEZAJI WA SIMBA MJITAMBUE. MNAPOCHEZA TAFUTENI KWA NGUVU ZENU ZOTE NAFASI YA KUFUNGA NA WAFUNGENI HATA MAGOLI 10 . MSIPIGE MIPIRA YA PASI TUU MPAKA MNAMCHEZESHA KIPA NAE APIGE PASI. ROUND YA PILI TIMU HIZI ZITATUBADILIKIA TUTAPOCHEZA KWENYE VIWANJA VYAO. SIMBA TUNAKAMIWA NA KILA TIMU. MSIJISAHAU WACHEZAJI.
ReplyDeleteSALAMBA AMEFANYA UBISHOO GANI JANA AMEINGIA DAKIKA ZIMEBAKIA CHINI YA 10 ALIGUSA MPIRA ZAIDI YA MARA MBILI KWA MUDA ALIOINGIA AMEJITAHIDI NA HAKUFANYA UBISHOO WOWOTE TUSIMUONEE. HAPAKUWA NA PENETI USEME KAMPASIA KIPA. BIG UP SALAMBA WEKA KASHKASH KULE MBELE KILA UNAPOCHEZA PIGA MASHUTI TUUU MAGOLI UTAFUNGA.
DeleteHapo kwakweli sijakuelewa salehe jembe
DeleteHawa vijana wadogo mnawalaumu bure.Kuna shida sehemu. Ushindi unaopatikana ni wa kubahatisha bahatisha tu. Timu haichezi vizuri. Wachezaji hawajitumi ipasavyo. Mi nafikiri hata malipo ya mchezaji yangeendana na namna anavyojituma uwanjani.Kuna haja gani ya kuwalipa wachezaji mishahara mikubwa wakati hawajitumi uwanjani.
ReplyDeleteWacha utani, Kagere, Okwi, Erasto Nyoni, Wawa, Bocco ni vijana!!!
DeleteKama unatak vijan nenda serengeti boys
DeleteLigi ikiwa haina ushindani watu wanalalamika. Ligi ikiwa na ushindani watu wanalalamika. Akili za watanzania kama vile zimetengezwa kutokana na madin ya matope. Watu inabidi waipongeze Simba kwa upata ushindi na pia kufurahia kiwango kilichooneshwa na prisons. Hata kocha wa Taifa Stars kama aliangalia mechi nadhani bila ubishi ameshuhudia mwenyewe viwango halisi vya wachezaji wa Tanzania kwani takribani wachezaji wote wa Tanzania prisons ni wazawa.
ReplyDeleteWell said brother, mi kwa kumbukumbu zangu prisons ni timu ngumu mnoooo, wachezaji wake wako fit mnooooo, nawapongeza sana Simba kwa kupata hata huo ushindi wa goli moja, wale jamaa wako composed mnooo, kama wakiendelea vile wanafika mbali, mwaka jana walikuwa wa 4 na kuna timu kubwa zilikufa sokoine na wale jamaa walishinda hata nje ya sokoine. Wanao ongea na kubeza ushindi huo hawajui mpira, kwa soka la bongo kuna timu kama Mtibwa, Prisons, Azam ni timu ukikutana nazo ujipange, sijajua JKT Tz na wengine. Singida united inaanza kupotea. Tusubiri ligi bado mbichiiiii
DeleteBinafsi nimeangalia mechi za Simba hasa ile ya Mtibwa na ya jana ya Prison. Ninachokiona uchezaji sio mbaya. timu inacheza vizuri sana first half inatiririka/kuunganika vizuri kuanzia beki hadi ushambuliaji. Kipindi cha pili timu inatumia mipira mirefu na hivyo kuruhrsu kushambualiwa. kinachohitajika ni kujenga physique ya midfield hasa ile ya kushambulia ili muda wote timu isichange pattern ya mchezo. Vile vile maamuzi na muda sahihihasa eneo la mble ya katikati linahitaji kufanyiwa kazi. Otherwise timu ni nzuri kikosi kipana na talent binafsi za wachezaji ni safi. Tuwape muda
ReplyDeleteUmeongea vizuri Simbadamu,wewe umeisoma vizuri timu,tuwape muda.
ReplyDeleteMwandishii ajui kitu
ReplyDelete