August 23, 2018


Na Haji Manara

Wakati mwingine najiuliza nn wanadaamu wanataka?hasa washabiki wa Mpira!!

Nimetalii kdogo kwenye magroup machache ya Wanasimba kwenye WhatsApp nimeshangaa baadhi yetu kutokuridhika na ushindi wa leo wa goli moja dhidi ya Prisons

Wengine kwenye Instagram wanafika mbali zaidi eti mfumo wa kocha haufai!! 

Guys mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kumfanyia upasuaji wa kichwa mtu,ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba hujui mpinzani wako kajipangaje..hujui kama siku hyo wachezaji wako watacheza kwa kiwango gani lakini kubwa Sayansi hii haina jawabu la moja kwa moja kama hesabu au hisabati 3×3 ni tisa tu, hata ukokotoe vipi! Huku kwetu kwenye ndiki 3×3 inaweza kuwa bilioni nane.

Mara nyingi huwa nakataa kuwepo kwenye groups za WhatsApp sababu asilimia kubwa mpira wameujulia mitandaoni..hawana shibe ya mchezo huu adhimu kabisa!!

Kwao hudhani kila siku Simba itashinda na kwao ushindi ni lazma upate goli saba au tano..kwao ushindi ni mnono tu..hata kama unakutana na Wanaume wenzako!

Wanabeza huku wakisahau Prisons iliingia top four Msimu uliopita,wanabeza huku wakijua Prisons haifungwi kitoto kama Mnyela United!

Halaf wanakuja na hoja dhaifu inayopaliliwa na wanazi wa nazi chai eti team imetoka Uturuki why ishinde moja? Afana aleik!!

Hapo ndio Haji naonekana mtata aliowaambia tulienda Uturuki kujifunza mpira ni nani? Kule tulienda camp ya pre season.ni mazoezi ya mwanzo wa msimu
Wengine walienda Zanzibar kama Prisons na wapo walioenda hadi Mkamba kote huko ilikuwa inatafutwa chemistry ya timu toka kwa makocha.

Ni lazima mnapoamua kuushabikia mchezo huu mjifunze sayansi yake na msijifunze sayansi hii kiwepesi wepesi kama mnajifunza Sayansi kimu 

Leo tumecheza na team nzuri na walijiandaa kama tulivyojiandaa sisi na lazma muelewe mfumo wa kocha hauingii kwa kipindi kifupi, unachukua muda kdogo

Niwasihi sana Wanasimba Soka ni zaidi ya mchezo wa drafti au Chess ya kina kasparov na karpovi nahitaji shabiki kabla ya kulaumu ajue vtu vingi kdogo kwenye medula yake, vinginevyo ni kufanya uchale tu.

Sina maana tunakataa ushauri ila uwe ushauri unaoendana na taaluma na kama huna jijengee busara ya kupiga kimya, usifate mkumbo wa mitandaoni 

Mwisho niwasihi tena na tena cc washabiki kazi yetu ni mbili tu, sapoti na Dua na Sala, mengine ni kujitafutia kisukari kama si Pepopunda!

15 COMMENTS:

  1. MIMI NIKUSIHI MANARA USIWAZUIE MASHABIKI KUTOA HISIA ZAO NA WALA USIDHARAU MAONI YAO. WANAYO HAKI YA KUTOA MAONI YAO. KAULI ZA KUWABEZA ZITAHARIBU UMOJA WETU NA KUTOA MWANYA KWA TIMU YETU KUTOFANYA VIZURI. JIKUMBUSHE KANUNI ZA UONGOZI NA UTAWALA BORA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. KLABU NI YA WATU WENGI HII IMEANZA MWAKA 1936 IN WANACHAMA NA MASHABIKI MIAKA YOTE HIYO HIVI WOTE WAWE NA MAWAZO SAWA NA YAKWAKO MANARA? HAIWEZEKANI. KUTOFAUTIANA MAWAZO NDIO KUJENGA CHETU. WALA USIWAPUUZE NA KUDHOOFISHA WANACHOHOJI NA KUSHAURI. WALA USIWADHARAU. WASIKILIZENI. VIONGOZI NDIO WAJIBU WENU.

      Delete
  2. Wakati vyombo vya habari vinaisifia hii timu ulisapoti. Leo watu wanasema haichezi vizuri hutaki watoe maoni yao. Mpira wa miguu ni mchezo wa hadharani. Kila mtu anaona kiwango kibovu kinachooneshwa na timu. Wasisitize wachezaji wajitume badala ya kuponda watu.

    ReplyDelete
  3. Manara aliugua uchizi kwahiyo kama kiwango kibovu cha timu wasihoji juu ya timu Yao wacha watu waongee timu sio ya Baba yako mzazi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msimzonge sana Manara yeye ni Mwanasiasa na siasa ameirudisha mpirani, hivyo mnapaswa kutambua hivyo na kumlaumu ni kumuonea.

      Delete
  4. Manara yupo sawa kabisa na wanamuuona chini basi wajue muda si mrefu wakajikuta wapo kwenye jelea waendawazimu. Manara anazungumza facts na kwa watu wenye vichwa vya kuku kwa kufikiri basi watapata tabu sana kwa Manara. Tanzania prisons hapana shaka yeyote walitoka Zanzibar na kuingia uhuru pale Dar wakiwa wamejizatiti kisawasawa kwenda kuifunga SIMBA matokeo yake wameambulia kichapo sasa atakaeibeza Simba atakuwa anamatatizo ya akili. Binafsi nawavulia kofia Simba kuondoka na ushindi mbele ya prisons kwani wanaokena wapo fiti hasa na kama prisons wataendelea kucheza kwa kiwango kile basi nawatabiria makubwa ila tofauti ya SIMBA na timu kama prisons kila ligi ikisonga mbele utagundua Simba kiwango kinapanda na nyengine kushuka viwango ila timu zote za ligi zinatakiwa na ushindani wa maana ili kuinua soka letu.

    ReplyDelete
  5. Tumuache kocha na benchi la ufundi wafanye kazi yao. kama kuna mtu anaona kocha hafai na apeleke cv zake ili akapewe kazi hito. kama tumeshinda mnalaumu mnatakaje? Tuwe na Subra.

    ReplyDelete
  6. Manara yupo saws,timu haikwenda haikwenda uturuki kujifunza soka lakini utashangaa waandishi na watangazaji uchwara wakisema ama wakita simba ya uturuki kwa kebehi,huo no ushamba

    ReplyDelete
  7. Mbona Simba wapo fresh tu. Wanapendeza kuwaangalia jinsi wanvyotandaza soka safi hasa katika hii mechi na Prisons Simba wameupiga mpira wa hali ya juu yaani soka ya uhakika na kama washambuliaji wake wangekuwa makini Mjela angekufa si zaidi ya goli nne safi. Cha kufanya wachezaji wa Simba hasa washambuliaji ni kutulia wanapofika golini lakini huwezi kujua prisons wametokea Unguja katika safari yao pengine wameambatana na mtaalam asilia wa masuala ya upepo:)
    Kitu kimoja cha kushangaza ni umbile kubwa alilonalo Kagere na jinsi anavyonyumbulika kama treni ya umeme kwaweli Simba imeramba dume pale.Viongozi wa Simba waliofanya usajili mara hii wanastahiki pongezi.

    ReplyDelete
  8. Kwani Haji Manara sayansi ya mpira kaijulia wapi kuzaliwa na Sunday au kukulia Kariakoo? Mbona tunamjua sana tu. Acha watu wawe huru ndo maana ya uhuru wa kutoa maoni.
    Simba yenye usajili wa mabilioni na benchi aghali la ufundi ni ya kuhenyeshwa na timu ambayo imesajili wazawa tupu, nini advantage ya kusajili wachezaji wa nje 10 waliopo Simba kama timu kutoka Mbeya inaweza toa upinzani mkubwa kimchezo na kiufundi kiasi kile?
    Haya yalianzia kwa Mtibwa na yameendelezwa kwa Prisons. Tusije kuchelea mwana kulia
    Manara akumbuke Simba ni ya watu wengi na yeye hana mamlaka ya kuhodhi mijadala, ni msemaji tu wa Kamati ya utendaji au bodi ya Simba. Angalizo kuu mi kwamba kati ya wanaochangia kwenye mitandao anaowabeza, wana elimu kuliko yeye na wameucheza mpira mwingi tu. Wabillah taufiq

    ReplyDelete
  9. Si ulipiga kelele weee timu 1 B sasa!

    ReplyDelete
  10. mfumo mbovu 3-5-2 ndo unafaa kulnda na kushambulia kwa kasi 4-4-2 ni wa kuzia

    ReplyDelete
  11. Au kweli kule uturuki walikua wanacheza na madeleva taxi

    ReplyDelete
  12. Au kweli kule uturuki walikua wanacheza na madeleva taxi

    ReplyDelete
  13. Utasema sana, chess ni sayansi kubwa sana, ndio maana game moja inaweza lala hata siku 3 haijaisha. Mpira upo na sayansi yake ni kweli lkn makosa yenu hasa wewe Manara maana uliwajaza upepo sana mashabiki ili kuwaaminisha mliosajili ni malaika na sasa ndio unakumbuka umesajili binadamu? Endelea kuchezea hela za Mo kwa kusajili majina na kuwafanya mashabiki wako waamini umeleta Ronaldo au malaika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic