August 5, 2018


Wakati wadau, wanachama na mashabiki wa Yanga wakianza kuichangia klabu yao ikiwa ni baada ya uongozi kutoa namba maalu, Tawi la Yanga Temeke limesema litatoa fedha zake kwa sharti moja.

Tawi hilo limesema kuwa wamekubaliana kwa ujumla kuisaidia Yanga japo wakitaka ni vema kuwe na uwazi wa matumizi ya fedha hizo na badala yake zisiishie mifukoni mwa watu binafsi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tawi hilo, Mustapha Mohammed, ameeleza kuwa Yanga wanapaswa kuweka wazi juu ya matumi ambayo yatafanjwa mara baada ya wao kuchanga fedha kutoka kundi lao.

Mustapha amefunguka na kueleza ni vema ikawa hivyo ili kuondoa mkanganyiko wa mambo juu ya matumizi ya fedha hizo kutokana na klabu kuwa katika hali ngumu kifedha.

"Sisi kama tawi la Yanga Temeke tumejipanga kuisaidia klabu yetu kwa kuichangia lakini tunataka kuwe na uwazi wa matumizi ya fedha hizo ili zisije zikaishia mikononi mwa watu binafsi" alisema Mustapha wakati akizungumza na kipindi cha Radio One, kupitia Spoti Leo.

4 COMMENTS:

  1. Wasaidieni kwasababu wana njaa na wala msiombe uthibitisho wa hesabu, mmekubali basi ni bora mnyamanzi na ikiwa kweli mnaipenda yanga basi pia muwapende viongozi wake na mambo kusitiriana na kama hawatapata mlo vipi wataitumikia timu

    ReplyDelete
  2. Hata we Leo hii utasema aibu ya wanayanga lkn kumbuka hii ni timu wananchi na wanawakilisha TZ kwhyo kuweni wapole na maneno yenu

    ReplyDelete
  3. Hata we Leo hii utasema aibu ya wanayanga lkn kumbuka hii ni timu wananchi na wanawakilisha TZ kwhyo kuweni wapole na maneno yenu

    ReplyDelete
  4. Yanga ndio CCM Vipi CCM imefilisika!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic