LICHA YA KUWEKA KAMBI UTURUKI, SIMBA WAPIGWA MKWARA MZITO MROGORO
Wakati kikosi cha Simba kikitarajia kuanza safari ya kurejea nchini baada ya kambi ya wiki mbili kumalizika huko Uturuki, uongozi wa Mtibwa Sugar umezidi kuwatumia mabingwa hao wa Ligi Kuu salaam za moto.
Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, amesema kuwa kuelekea mechi ya Ngao Ya Hisani itakayopigwa Agosti 18 2018 kwenye Uwanja wa CCm Kirumba, Mwanza, hawababishi na kambi hiyo.
Kifaru ameeleza kambi ambayo Simba wameweka ni sawa na kujipotezea muda bure hivyo pale watakapokuja kucheza na Mtibwa watarajie kichapo.
"Unajua Simba wamekuwa na mbwembwe nyingi sijui wapo Uturuki, sisi tunawaahidi kichapo cha maana katika mchezo wa Ngao ya Hisani, tunawasubiria warejee" alisema.
Baada ya kichapo cha mbwa koko msitokee kwa mlango wa nyuma.
ReplyDeleteNguvu1
ReplyDeleteMwenzake Masau Bwire alisema hayo hayo akala kipigo akatoka uwanjani saa mbili usiku na akatukuta wanaume tunamsubiri na tukampa maneno yake akaea mdogo kama piriton
ReplyDelete