Kamati ya Uchaguzi kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeitaka klabu ya Yanga kufanya uchaguzi mkuu badala ya kujaza nafasi za viongozi ambazo zimeachwa wazi, imeelezwa.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya uongozi wa klabu hiyo hivi karibuni kuibuka na kusema utajaza nafasi za baadhi ya viongozi ambao wamejiuzulu huku nafasi ya Mwenyekiti ikibakia kama ilivyo.
Taarifa inaeleza kuwa, Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ndani ya Yanga, Bakili Makele, hivi karibuni alisema Yanga haitafanya uchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti kutokana na kumtambua Mwanachama wake na Mfanyabiashara, Yusuf Manji kuendelea kukaa kwenye kiti hicho.
Makele alieleza hayo akisema wao kama klabu watajaza nafasi pekee ambazo zimeachwa na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
Kutokana na maamuzi hayo, TFF imewajia na kuwalazimu wafanye uchaguzi mkuu ikiwemo kupata mbadala wa nafasi ya Mwenyekiti Mkuu ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Manji ambaye alijiuzulu nafasi hiyo.
Wapewe nafasi ya kuzidi kumuangukia miguu yanga kwasababu yeyote mwengine wataempata hatokuwa tayari kuuangamiza utajiri wake kama alivofanya Manji na ushahidi umeonekana kuanguka kwa yanga kifudifudi baada ya Manji kuiacha mkono. Hakuna pesa ya Manji manaake hakuna ufalme wa yanga tuliouzoea. Pia kwa upande mwengine ukifanywa uchaguzi wa kumpata raisi mpya na ikiwa kweli Manji anautaka uraisi na yuko tayari kumwaga tena mabilioni, hapana ataemzuia kutetea uraisi wake.
ReplyDeleteYupo Manji, kama hawezi tena kurudi aje Tarimba. Hatuwezi kuyumba.
DeleteTFF walisema wanamtambua Manji ndio mwenyekiti wa Yanga wakamuondoa Sanga kwenye nafasi ya uenyekiti wa bodi ya ligi LEO HAWAMTAMBUI TENA MANJI KAMA MWENYEKITI!!? Soka kukua Tanzania kwa viongozi namna hii aidha itachukua muda ama itokee miujiza
ReplyDelete