Vijana wa Tanzania, Serengeti Boys watacheza kuwania mshindi wa tatu katika michuano ya Kombe la Cecafa chini ya miaka 17 baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Uganda.
Uganda ambao wamekuwa wakilalamikiwa na makocha kadhaa kuwa na wachezaji vijeba, wameifunga Serengeti Boys kwa mabao hayo 3-1 kwenye mchezo wa nusu fainali kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Katika mchezo huo, mabao ya Uganda yalifungwa na Abdulwahid Iddi, John Alou na la tatu Alphonce Msanda akajifunga huku lile la kufutia machozi la Serengeti Boys lilifungwa na Edson Mshirakandi aliyechonga kona moja kwa moja.
Kwa ushindi huo, Uganda watawavaa Ethiopia katika mechi ya fainali huku Serengeti Boys wakissubiri kucheza kuwania mshindi wa tatu dhidi ya Rwanda waliofungwa kwa penalti 4-2 na Ethiopia baada ya sare ya 2-2 katika muda wa kawaida.
0 COMMENTS:
Post a Comment