UMAFIA ITAKAOTUMIA REAL MADRID KUMTWAA MBAPPE HUU HAPA
Real Madrid bado inafanya mbinu za kimafia ili kumsajili straika wa Paris St. Germain (PSG), Kylian Mbappe. Klabu hiyo inasubiri hatma ya shauri la PSG lililoko kwenye Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) ambako inakabiliwa na tuhuma za kukiuka kanuni za fedha za shirikisho hilo.
PSG inatuhumiwa kununua wachezaji kwa bei mbaya wakati fedha wanazoingiza za udhamini ni kiduchu. Katika kudhihirisha kuwa Real ina mkono wake katika suala hlo, uongozi wa La Liga kupitia Rais wake, Javier Tebas ndio umewasilisha malalamiko UEFA kuhusu suala hilo.
Ikiwa PSG itaadhibiwa ina maana italazimika kuuza baadhi ya nyota wake, ambapo sasa Real Madrid inatega hapo kumpata Mbappe, ambaye aliitikisa duniani baada ya kuiongoza Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia.
Hapo ndio Real Madrid inapotegea kwani inaona kuwa itampata Mbappe kwa bei ya mteremko. Uongozi wa Real Madrid umeandaa kitita cha pauni milioni 180 ili imnunue ikiwa PSG itaadhibiwa na UEFA. Dirisha la usajili katika nchi za Hispania, Ujerumani na Ufaransa linatazamiwa kufungwa Agosti 31, mwaka huu wakati uamuzi wa UEFA utatolewa Agosti 30.
0 COMMENTS:
Post a Comment