SIMBA WAJIFUNZE KUHESHIMU TIMU NYINGINE
Ni raha ya shabiki timu yake kusheheni mastaa wakubwa kwenye mchezo husika kutoka sehemu mbalimbali, lakini hiyo siyo tiketi ya moja kwa moja ya kupata matokeo.
Lazima tujifunze kuheshimu timu pinzani, hii ni soka na matokeo yanatokana na kile unachokifanya ndani ya dakika 90. Haya maneno mengine ya nje ya uwanja ni mbwembwe.
Mashabiki na wadau waache kocha na wachezaji wafanye kazi yao uwanjani. Ishu ya Simba kuweka kambi Uturuki, Prisons kuweka Tukuyu au Yanga kukaa Kilosa ni sehemu ya maandalizi tu, ambayo mwisho wa siku hayahusiani moja kwa moja na kile kitakachotokea uwanjani.
Mchezaji anaweza kukaa kambini sehemu tulivu akapata kila kitu lakini mwisho wa siku kutokana na uzito wa mwili au ugumu wa mazoezi aliyokuwa anapata ikamchukua muda kutoa matokeo chanya uwanjani ambayo mashabiki wanayo vichwani mwao. Ishu ya msingi kwenye ligi haswa katika hatua za kwanza kama ilivyo sasa ni pointi. Magoli siyo ishu sana, Simba wabadilike wajifunze kuziheshimu timu nyingine.
Hata wangeifunga Prisons mabao 20 bado pointi zingekuwa ni zilezile tatu tu. Na lazima watambue kwamba Prisons siyo timu mbovu, ni timu ambayo ina wachezaji wengi vijana wenye uchu wa mafanikio na wenye nidhamu ya mchezo ambao wamekaa pamoja kwa muda mrefu.
Prisons inacheza kitimu zaidi iheshimiwe kama mpinzani, waliokuwa wanafuatilia ule mchezo haswa kipindi cha pili waliona Prisons ilichofanya. Siyo timu ya kubeza au ya kwenda uwanjani ukiwa na matokeo yako mfukoni. Tujifunze kuheshimu kazi za watu wengine.
Mashabiki wampe muda Kocha wa Simba afanye kazi yake, yule wa Prisons amekaa muda mrefu sana na timu yake na hata msimu uliopita alifanya vizuri na kuwa kocha bora.
Ligi ndiyo kwanza inaanza mashabiki waache papara na maneno ya kukatisha tamaa wachezaji, wawape morali tuone ligi ya maana na soka lenye ushindani. Bado safari ni ndefu, jifunzeni kuheshimu wapinzani.
Na Mzee wa Kutibua
Simbwa bwana...
ReplyDeleteMimi siamimi kama wanaolalamika mitandaoni na kwengineko kuwa Simba imefunga magoli kiduchu katika mechi yake ufunguzi kuwa kweli ni mashabiki wa SIMBA? Yawezekana kabisa kuwa ni mashabiki maamluki wenye lengo la kuivuruga na kuitoa timu mchezoni. Na kama kweli ni mashabiki wa Simba wanaolalamika basi wanatakiwa kutubu kabla hawajatubishwa. Tumehuhudia jana Liverpool wakipata ushindi mwembamba nyumbani kwao na timu ambao si miongoni mwa Top 4 au Manchester city kulazimishwa suluhu na kitimu cha kawaida. Liverpool ni timu ilyofanya usajili wa kubeba champion league lakini sio kigezo kwamba isipate upinzani katika ligi ya Uingereza hasa kwa zile timu ambazo ni za kawaida. Hata Barcelona hutokea kufungwa na vitimu vya kawaida sana na ndio mpira. Wanaosema kuwa mbona mwaka jana Simba ilipata ushindi wa kishindo katika mechi yake ya ufunguzi? Ni ujinga mtupu, Mwaka jana mkamerooni ulikuwa msimu wake wa pili na timu na alikuwa anakutana na Ruvu shooting. Hata mazingira ya mentality ya akili za watanzania wengi katika utendaji wa kazi zimebadilika sana katika zama hizi za Magufuli tofauti kabisa na hapo awali hicho ndicho ninachokiamini mimi na si ajabu tukaona upizani mkali kutoka kwa timu zilizo chini ya taasisi za serikali. Kitu kimoja tu sio siri Simba imekusanya mastaa wa rika mbali mbali na wapo pahala sahihi kabisa kwa wao kufanya kazi yao kwa utulivu.Sasa wachezaji wa Simba wanatakiwa kuelewa hilo kwani kuna wachezaji kadhaa wangetamani kucheza katika mazingira ambayo wachezaji wa Simba wanayo kwa hivyo Simba wajiandae kwa upizani wa kweli kutoka kwa timu nyengine la sivyo watakuja azirika na ustaa wao. Ni kichekesho kusikia mchezaji wa Simba eti kaishiwa pumzi mbele ya mchezaji wa Yanga ambae hata kiakili hayupo vizuri kutokana na ukata. Simba ni miongoni mwa professional like a team ukanda huu wa Africa mashariki suala la pumzi kwa mchezaji sio suala la kocha ni la mchezaji binafsi kujitambua na kwa kweli ni vitu vya kushangaza sana kwa vijana wetu kutokuwa makini na hilo.
ReplyDeleteHuwezi kukataza mashabiki kusema ovyo ndio kazi yako.Wanataka timu ishinde bila kutilia maanani kwamba baada ya mapumziko marefu timu ilikwenda Uturuki kwenye preseason nä kufanya mazoezi magumu. Kocha ni mgeni anahitaji muda kujenga falsafa yake.Timu inaendeshwa kisasa sana kuliko wakati wowote katika historia ya Simba.Wanachama na wapenzi timu upp kwenye mikono salama hamna haja ya kuwa na wasiwasi.
ReplyDeleteHata Yanga waheshimu timu zingine..Baada ya kushinda mechi mbili mfululizo wanaona ndiyo walishakuwa mabingwa.Wakati takwimu zinaonyesha mechi zote mbili wameshinda kwa bahati..Hubahatiki siku zote
ReplyDeleteSawa kabisa. Timu zote ziheshimiane. Ligi ndio kwanza imeanza.
Delete