August 29, 2018


Na George Mganga

Kocha mkuu wa Timu ya Tanzania, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amewaondoa wachezaji 6 wa Simba  kwa kosa la kuchelewa kuripoti kambini isipokuwa Mlindalango Aishi Manula.

Wachezaji hao isipokuwa Manula aliyewahi kambini, walitakiwa kuripoti siku ya Jumatatu baada ya kumalizika kwa mchezo wa dhidi ya Mbeya City lakini walishindwa kufanya hivyo.

Wachezaji hao ni Nadhodha John Bocco, Shiza kichuya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe pamoja na Hassan Dilunga.

Kwa upande wa viongozi wa Simba ambao ni Meneja wa Klabu, Richard Robert ,pamoja na Kaimu Katibu Mkuu, Hamis Kisiwa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  limewapeleka kwenye Kamati ya Maadili kwa kutotimiza wajibu wao.

Baada ya kuondolewa, wachezaji walioitwa kuchukua nafasi zao ni Paul Ngalema wa Lipuli FC, Salumu Kimenya wa Tanzania Prisons, David Mwantika na Frank Domayo wa Azam FC, Salumu Kihimbwa na Kelvin Sabato wa Mtibwa Sugar na Ali Abdulkadir.

18 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usiite mwanadamu mwenzio mbwa MUNGU anakuona utapata laana

      Delete
  2. Safi sana.....kocha ameonyesha weledi wa kazi yake,tatizo wachezaji wetu wa kibongo hasa wale mastaa wanajiona miungu watu kiasi wanaweza kupindisha taratibu za kocha au viongozi wao wengine.

    ReplyDelete
  3. Nidhamu kwanza,Lazima wajue kuwa Taifa stars in Brand Kubwa...

    ReplyDelete
  4. Safi sana, itakuwa fundisho kwa wengine.

    ReplyDelete
  5. Mbona kama maamuzi ya kukurupuka.kwani kuliwekwa deadline yaani muda maalum wa kuripoti kwa wachezeji au maamuzi ya kinguvunguvu tu?

    ReplyDelete
  6. Huyo kocha mbwembwe zake zitamponza. Kaye happy wachezaji ni muhimu stars kutokuwepo kwao atajajutia. Anatengeneza mgogoro bila sababu ya msingi. Mimi naona kuna hujuma TFF wanapanga dhidi ya samba. Fikiria wamecheLewa dawa, hata hawajaitwa kujitetea lakini wengine washateuliwa na kwenye kamati ya maadili washapelekwa ni kichekeshooo. Aibu! Kwani wengine walioitwa wameripoti Wote??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo hatukuzoea tuatazoea, kama walikuwa na matatizo wao ndyo walitakiwa kutoa taarifa sio kusubiri kuulizwa kwa nini wamechelewa. Tujifunze kuheshimu taratibu.

      Delete
    2. Hatujengi tunabomoa. Umoja utakosekana .

      Delete
  7. Kocha kakurupuka. Simba kaeni na wachezaji wenu.Kwani hata wakiumia TFF haiwatibu. Aliumia Shomari Kapombe ikabidi Simba wamtibu. Kocha akazie msimamo wake asije akawaita baadaye.

    ReplyDelete
  8. Safi Sana tunahitaji kocha wa namna hiyo.hakuna mchezaji aliye juu ya kocha. Hilo liwe fundisho kwa wengine. Nina imani kwa mtindo huu nidhamu itakuwa ni yahali ya juu Sana na tutasonga mbele.

    ReplyDelete
  9. Lazima ilitokea kutokufahamiana. Wachezaji waliofekwa ndio uti wa mgongo wa timu ya taifa. Hasira hasara. Ikiwa walitenda kosa na kwa jinsi hali ilivyo na kwakua kocha ni mpya, haikubidi iwe hatuwa yake ya kwanza kutimuwa bali angetumia hekima angalau kuwapa onyo kali wachezaji hao. Kosa la kwanza haliwachi mke na hasira ni hasara. Pstience is bitter, but its fruits are sweeter

    ReplyDelete
  10. Iyo nimeupenda na kocha aendelee na msimamo wake huo ,ebu tujiulize hili LA kuchelewa ni kwa wachezaji wote wa taifa staa? VP kuhusu samata,msuva n.k

    ReplyDelete
  11. Safiiiiiiiii kochaa timua hizo mbwaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  12. Matembele hamna lolote, kocha gani? Huko kwao Nigeria wachezaji wote wakiitwa timu ya Taifa hufika kwa pamoja?

    ReplyDelete
  13. Hata kama yupo right basi atakuwa anakosa busara. Shabiki au mashabiki wanahesabika kama mchezaji wa kumi na mbili. Taifa Stars uwanja wake wa nyumbani ni uwanja wa taifa Daresalam. Kuwaondoa wachezaji wa Simba timu ya Taifa ni kuwafukuza mashabiki wa Simba uwanjani, yaani pumba kabisa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic