August 26, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Singida United umesema kuwa hauna hofu na Kocha wake Mkuu, Hemed Morocco kuitwa katika timu ya taifa, Taifa Stars.

Morocco ameitwa kwa ajili ya kumsaidia majukumu Kocha Emmanuel Amunike akiwa kama Msaidizi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Uganda utakaopigwa hivi karibuni kwa ajili ya kufuzu fainali za kuelekea AFCON.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Singida, Festo Sanga, amesema kuwa kitendo cha Morocco kuitwa Stars ni jambo la baraka kwao kutokana na mchango wake kuthaminika.

Morocco atakuwa anawajibika na Stars kwa kipindi ambacho timu hiyo itapaswa kuanza maandalizi ya kuelekea mechi hiyo dhidi ya Uganda huku akiitosa kwa muda Singida.

Stars itashuka dimbani kumenyamana na Uganda Septemba 8 2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic