August 14, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa Yanga umeweka hadharani kiasi cha fedha ilichopokea kutoka kwa wadau wake ambazo ni za mchango kwa ajili ya kuisaidia klabu.

Hivi karibuni Yanga kupitia Kaimu Katibu wake, Omary Kaaya, alitangaza kuanzisha utataribu wa kuichangia klabu ili iweze kuendesha shuguli zake muhimu kutokana na kupitia kipindi cha mpito.

Katika siku nane za mwanzo kuanzia Agosti 2 mpaka 10, Yanga imepokea kiasi cha shilingi za kitanzania 3,073,263.



Hata hivyo mabosi wa Yanga wamezidi kuwaomba wapenzi, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuzidi kuichangia klabu ili iepukana na hali ngumu ambayo inapitia kwa sasa ili mambo yazidi kwenda sawa.

5 COMMENTS:

  1. Duh kelele zote huku mtaani siku 8 million 3 tu nasisi ndio wamiliki wa timu kwa asilimia 51 kweli tutafika

    ReplyDelete
  2. Tafadhali, tunaomba maelekezo ya jinsi ya kuchangia.

    ReplyDelete
  3. Tunawaomba wanayanga wawe na moyo wakuisaidia timu kifedha na wala si maneno matupu tu. Kwa timu kama yanga ni aibu tupu kwa muda huu wote kupatikana milioni tatu. Bora tungenyamaza kimya kuliko kuonesha udhaifu tulionao. Juu ya yote haya ni bado kuwa tunajipanga kuizomea Simba, huko si ndio tunazidi kujiangamiza? Inaonesha wazi kuwa wachoyo hatupo tayari kuinyooshea mkono timu yetu

    ReplyDelete
  4. Majina yetu hayaonekani nitajuaje kama mchango wangu umejumuishwa? Wekeni wazi majina ya wachangiaji

    ReplyDelete
  5. Lakini inaingia akilini pesa zilizopatikana ni hizo tuuu na dasturi katika michango huandikwa majina waliochanga pamoja na ukubwa wa mchango wa kila mmoja lakini hayo hayakutokea, vipi tutaamini???

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic